Maagizo ya Rais Samia kwa NGOs...

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, ameyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kuongeza uwazi na uwajibikaji katika kazi zao pamoja na kwenda sambamba na vipaumbele na mipango ya Serikali ili ziweze kuleta tija katika jamii.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali Nchini (NGO’s) katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijji Dodoma leo Septemba 30,2021. 
Mhe. Rais Samia amesema hayo leo Septemba 30, 2021 wakati akihutubia katika Mkutano wa Mwaka wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
Mhe. Rais Samia amesema, kwa sasa Serikali inatekeleza Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2021/2026) hivyo ni vyema Mashirika hayo kuandaa mipango yake kwakuoanisha
na mpango huowa

 Serikali. Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima akimkabidhi Tuzo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa kutambua kazi kubwa anayoifanya katika kujenga Taifa la Tanzania, kwenye mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali Nchini (NGO’s) uliofanyika leo Sept 30,2021 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijji Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kuhusu utekelezaji wa mipango mbalimbali ya kazi za Mashirika yasiyo ya Kiserikali Nchini (NGO’s) alipotembelea mabanda ya maonesho katika mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali Nchini (NGO’s) uliofanyika leo Sept 30,2021 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijji Dodoma.  Aidha, Rais Samia ameyataka Mashirika hayo Yasiyo ya Kiserikali hususan ya ndani pamoja na Wizara husika kuandaa mpango mkakati utakaosaidia Mashirika hayo kuondokana na utegemezi katika utendaji wa kazi zao.

Mhe. Rais Samia ameyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kufanya kazi zinazoendana na mila, utamaduni, desturi na maadili ya kitanzania pamoja na kusimamia sheria zinazoongoza Mashirika hayo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akionesha Taarifa ya Kielektroniki ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali NGO’s kwa maendeleo ya Taifa katika mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali Nchini (NGO’s) uliofanyika leo Sept 30,2021 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijji Dodoma. (Picha zote na IKULU).

Vilevile, Mhe. Rais Samia ameyaomba Mashirika hayo kufanya kazi pamoja na Serikali katika kuwaelimisha wananchi kuhusu kushiriki zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika Agosti 2022, na kuwapa wananchi elimu ya tahadhari za kujikinga na UVIKO 19.
Share:

Tags:

Comments
Leave a Comment